“Zangu salamu zipokee”

Mkimwona ,
Mwambie zangu salamu azipokee
Kwa maana nyingi siku zimepita
Bila mawasiliano
Hivyo basi
Mkimwona,
Salamu zangu mwafikishie
 

Najua mchumba anaye
Maana ndo hayo mapenzi
Lakini
Mkimwona,
Mpitishie zangu salam
 

Zimekuwa miaka na mikaka
Siku zimepita
Miezi zaisha
Ilhali hatujaonana
Ndiposa nawahimiza
Mkimwona,
Zangu salam mwafikishie
 

Najua ulimi mmebarikiwa nayo
Hivyo mseme myasemayo,
Lakini mkimwona,
Zangu salamu azipokee
 

Haya mapenzi bana
Yatesa
Na ninajua si kupenda “kwako”
Wala si kupenda kwangu
Lakini najua wako mpenzi
Umempenda kwa dhati
Hata hivyo
Zangu salam zipokee
 

Kweli,
Msiba wa kujitakia
Kamwe hauna kilio
Maana nimeachwa nikilia
Laiti ningejua….
Hata hivyo
Zangu salam zipokee
 

Barua yangu naitamatisha
Ila msikose kumjulisha
Moyoni uchungu ninao
Maana
Nilipokonywa yangu dhahabu
Lakini msihi
Nafasi yake ungalipo
Iwapo ataona kurudi
Hata hivyo
Zangu salam azipokee
 

Kamwe sijakusahau hata kama umenisahau
Liwe kiangazi
Liwe masika
Moyoni ungalipo bado
Hivyo,
Tutaonana kwa mapenzi yake Maulana
Lakini
Zangu salam zipokee
 

Kwaheri Mpenzie